Chama, Kanoute waingia kinyang’anyiro mchezaji bora Afrika

Nyota wetu wawili ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Nyota hao ni Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao wanaowania tuzo hiyo pamoja na Mahmoud Kahraba na Pecy Tau wote kutoka Al Ahly.

Katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Horoya tulioibuka na ushindi wa mabao 7-0 Chama alifunga mabao matatu ‘hat trick’ akisaidia kupatikana kwa jingine moja wakati Kanoute akitupia mawili.

Zoezi la mashabiki kupiga kura linaendelea katika ukurasa rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.

Chama ndiye aliibuka mchezaji bora wa CAF wiki iliyopita na sasa anawania tena nafasi hiyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER