Chama, Bocco, Kapombe kuchuana mchezaji bora Desemba

 

Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Wachezaji hao ni kiungo mshambuliaji Clatous Chama, Nahodha John Bocco na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

Awali walikuwa watano pamoja na viungo Mzamiru Yassin na Pape Sakho lakini baada ya mchujo wamebaki nyota hao watatu.

Katika mwezi Desemba tumecheza mechi sita tumeshinda tano na kutoka sare moja huku nyota hao wakiwa ufunguo wa ushindi huo.

Mchanganuo wa takwimu zao za mwezi Desemba

Dakika Magoli Assist
Chama 540 4 7

Bocco 422 5 0

Kapombe 505 1 3

Zoezi la kupiga kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz litaanza leo saa 6:00 mchana litakamilika Januari 2 saa 6:00 mchana.

Mshindi atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi.

 

This poll has ended (since 1 year).
SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Naupongeza uongozi wa Simba kwa mikakati mizuri ya kuleta maendeleo ya timu na kutufurahisha mashabiki bila kusahau kuliheshimisha Taifa letu la Tanzania,Ili kuhakikisha kikosi kinakuwa imara kuelekea hatua ya makundi nawaombeni viongozi washushe vyuma 3 vya maana yaani beki 1,kiungo mkabaji mmoja na striker namba 9 mmoja..na wachezaji amabao Hawana ubora wa kuchezea Simba waondoeni na wengine watoeni kwa mkopo …..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER