Kiungo mshambuliaji Clatous Chama amerejea kikosini katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kukosekana kwenye mechi tatu kutokana na kutumia adhabu.
Kocha Juma Mgunda amempanga Chama kushambulia kutokea pembeni pamoja Augustine Okrah kwa sababu leo ameanza na washambuliaji wawili.
Baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi, Nahodha John Bocco ataongoza mashambulizi pamoja na kinara Moses Phiri.
Kikosi Kamili Kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Nassor Kapama (35), Kibu Denis (38).