Kiingilio cha chini katika mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza dhidi ya Jwaneng Galaxy kimepangwa kuwa Sh 5,000 kwa watakaonunua tiketi kwa njia ya kielektroniki huku siku ya mechi uwanjani itakuwa Sh 7,000.
Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwenye mitandao ya simu kupitia N Card hivyo mashabiki wanapaswa kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
Viingilio vingine ni VIP B na C Sh 20,000 wakati VIP A ni Sh 40,000.
Kwa mujibu wa utaratibu tulioelekezwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) mashabiki 15,000 pekee ndiyo wataruhusiwa kuingia uwanjani hivyo zoezi la kuuzwa tiketi litafungwa mara tu idadi hiyo itakapokamilika.