Bocco kuongoza mashambulizi dhidi ya Galaxy

Nahodha John Bocco amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa leo saa 10 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Hata katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Gaborone wikiendi iliyopita, Kocha Didier Gomes alimpanga Bocco kuongoza mashambulizi na kufunga bao la pili.

Bocco ataendelea kupata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Rally Bwalya, Bernard Morrison na Hassan Dilunga.

Katika eneo la ulinzi wa kati Gomes amewapanga Henock Inonga na Pascal Wawa wakati viungo wa ulinzi watakuwa Taddeo Lwanga na Sadio Kanoute.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Taddeo Lwanga (4), Bernard Morrison (3), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22) Rally Bwalya (8) Hassan Dilunga (24).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Peter Banda (11), Erasto Nyoni (18), Duncan Nyoni (23) Mzamiru Yasin (19),
Israel Patrick (5), Joash Onyango (16) Medie Kagere (14) Kennedy Juma (26)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER