Nahodha John Bocco atakabidhiwa kitita cha Sh 2,500,000 na Kampuni ya Emirate Aluminium baada ya kuibuka mchezaji bora wa mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Bocco ameonyesha kiwango bora ambapo amefunga mabao mawili kati ya matatu tuliyoshinda.
Emirate Aluminium iliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha kwa mchezaji bora wa mechi zote mbili za hatua ya robo fainali ikiwamo ile ya kwanza ya ugenini na hii ya leo ili kuongeza hamasa.
Emirate Aluminium ndiyo wadhamini wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki ambayo hutolewa kila mwezi na mshindi hupewa Sh 1,000,000.
One Response
Mnafanya vyema tunaomba muendeelee kutipa apdates