Benki saba zathibitisha kushiriki Simba Bankers Bonanza

Timu kutoka Benki saba zimethibitisha kushiriki Bonanza kubwa la (Simba Bankers Bonanza) litakalofanyika kesho katika kuanzia saa tatu asubuhi viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea mchezo wetu wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry utakaopigwa Jumatano, Benjamin Mkapa.

Timu hizo zimepangwa katika makundi mawili ambao timu mbili kwenye kila kundi itafuzu hatua ya nusu fainali.

Makundi hayo ni kama ifuatavyo

Kundi A

Equity Bank
Amana Bank
Stanbick Bank
NBC

Kundi B

TCB
NMB
Azania Bank

Bonanza la mwaka litakuwa la tofauti ya yale tuliwahi kuyafanya kuanzia Mfumo wa uendeshaji mpaka zawadi zitakazotolewa kwa washindi.

Bingwa atapata medali za Dhahabu, Kombe, seti ya jezi ya Simba tunazotumia kwenye michuano Kombe la Shirikisho Afrika na tiketi za mchezo wa Jumatano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER