Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema APR ni timu bora na imetupa kipimo kizuri na uimara wa kikosi chetu ulipo kwa sasa.
Benchikha amesema APR wanacheza vizuri kuanzia kwenye kuzuia mpaka kushambulia wapo vizuri kwenye kuziba mianya wakati wanaposhambuliwa.
Akizungumzia mchezo wenyewe Benchikha ameongeza kuwa ulikuwa mzuri na tulijitahidi kufanya kila tuliloweza kupata bao lakini tumekutana na timu bora.
“APR ni timu nzuri, inacheza soka safi. Ipo vizuri kwenye kuzuia pamoja na kushambulia lakini nasi tulikuwa vizuri ndio maana hakuna aliyefungwa.”
“Matokeo ya sare yalistahili kila timu ilikuwa bora, tunaenda kujipanga kwa ajili ya mchezo wa robo fainali,” amesema Benchikha.