Benchikha aridhishwa na viwango vya wachezaji

Pamoja na kupoteza kwa bao moja dhidi ya Wydad Casablanca katika mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wetu.

Benchika amesema kwa ujumla timu imecheza vizuri kuanzia kwenye ulinzi na kiungo lakini changamoto kidogo ilikuwa kwenye ushambuliaji kwakuwa tulitengeneza nafasi lakini hatukizitumia.

Benchikha ameongeza kuwa matokeo ya mchezo huo yametupa mwanga kuelekea mechi ya marudiano nyumbani na anaamini nasi tutapata ushindi na kuchukua alama tatu.

“Tumecheza vizuri, tuliweza kuzuia na kushambulia kwa kasi, eneo la kuweka mpira nyavuni ndilo tumeshindwa kufanikisha lakini nimeridhishwa na timu ilivyocheza.”

“Mchezo huu umeisha tunarudi nyumbani kujiandaa na mechi ya marudio ambayo tutajipanga vizuri na kuhakikisha tunakuwa sahihi zaidi ili nasi tushinde,” amesema Benchikha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER