Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye timu ndiyo sababu iliyotufanya kuchukua ubingwa wa ligi kwa mara ya nne mfululizo.
Barbara amesema kwenye mpira hakuna njia ya mkato bali ni uwekezaji sababu gharama za kuendesha timu ni kubwa.
Mtendaji huyo amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa uwekezaji alioufanya na kuifanya Simba kuendelea kuwa kubwa barani Afrika.
“Mafanikio ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo hayaji yenyewe bali ni uwekezaji mkubwa umefanyika na hili binafsi nampongeza Mo kwa kufanikisha,” amesema Barbara.
Barbara amesema kuelekea msimu ujao tutaendelea kusajili wachezaji bora na lengo ni kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tunataka kufika mbali Afrika, tutaendelea kusajili wachezaji bora ili kufanikisha hilo na hapa nyumbani hizi ‘back to back’ zitakuwa nyingi sana,” amesema Barbara.
2 Responses
Ni sahihi kabisa CEO,Bila ya kuwekeza hakuna mafanikio,angalizo katika usajili,tufanye usajili mdogo katika maeneo ya muhimu tu,Timu bado iko vizuri na uwezo wa kupambana Tena Kwa misimu kadhaa ijayo
GOOD JOB, ITS MY HOPE YOU WILL CONTINOUES TO GIVE US THE GOOD STAFF NEXT SEASON
SIMBA 4EVER.
GOD BLESS SIMBA MO EMPIRE, THE BEST YET TO COME