Winga Peter Banda amefunga bao lake la kwanza la mashindano akiwa na kikosi chetu katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Geita Gold uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.
Banda alitupatia bao hilo dakika ya tisa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kibu Denis kutoka upande wa kulia.
Baada ya bao hilo Geita walikuja juu kutaka kusawazisha lakini safu yetu ya ulinzi iliyokuwa chini na Kennedy Juma na Joash Onyango ilikuwa makini.
Mzamiru Yassin alitupatia bao la pili dakika ya 56 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Bernard Morrison sekunde chache baada ya kuingia kutoka benchi.
Dakika 66 Juma Mahadhi aliipatia Geita bao la kwanza kufuatia walinzi wetu wa kati kuzembea kuondoa hatari.
Kocha Pablo Franco aliwaingiza Bernard Morrison, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Medie Kagere na Pascal Wawa kuchukua nafasi za Ibrahim Ajibu, Rally Bwalya, John Bocco, Banda na Kibu.
Matokeo haya yametufanya kufikisha alama 17 baada ya kucheza mechi saba tukishinda mitano na sare mbili.
One Response