Baleke, Kibu, Ally wachuana Mchezaji bora Aprili

Wachezaji wetu watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao ni mshambuliaji Jean Baleke kiungo mshambuliaji Kibu Denis na mlinda mlango Ally Salim.

Katika mwezi Aprili tumecheza mechi tano huku nyota hao wakionyesha kiwango bora na kuwa na takwimu nzuri.

Hizi hapa takwimu zao za Aprili

Dakika Mabao Assist

Baleke 407 6 0

Kibu 450 1 3

Ally Salim amecheza mechi nne sawa na dakika 360 akifanikiwa kupata Clean Sheet tatu.

Zoezi la kupiga kura linaanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Mei 2 saa sita usiku.

Mshindi atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER