Awesu Awesu ni Mnyama

Kiungo mshambuliaji Awesu Awesu amejiunga nasi kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili.

Awesu amejiunga nasi akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na KMC aliyodumu nayo kwa miaka mitatu.

Awesu ni mchezaji mzoefu kwenye Ligi Kuu ya NBC na anaweza kumudu nafasi ya kiungo wa ushambuliaji na winga zote ingawa pia amewahi kutumika kama kiungo mkabaji.

Mbali na KMC, Awesu amewahi kutimikia timu za Kagera Sugar, Azam FC na Mwadui FC kwa nyakati tofauti.

Tumefanya marekebisho makubwa ya kikosi kwa kusajili nyota wapya ndio maana tunaongeza na wachezaji wazawa wenye ubora.

Kuelekea msimu mpya wa mashindano tunaandaa kikosi imara ambacho katika kila nafasi kutakuwa na wachezaji wenye ubora unaolingana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER