Alichosema Robertinho baada ya ushindi dhidi ya Vipers

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahishwa na kiwango tulichokionyesha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja.

Robertinho amesema kilichomfurahisha ni jinsi tulivyocheza kitimu hasa kipindi cha pili huku muunganiko wa wachezaji vijana na wazoefu ukiwa mzuri.

“Katika Ligi ya Mabingwa hasa hatua ya makundi ushindi ndilo jambo linalotakiwa, iwe moja, mbili au nne kinachoangaliwa ni pointi tatu.

“Tumecheza vizuri, tulikuwa na muunganiko mzuri mbinu yetu ilikuwa kuhakikisha tunapata ushindi, kipindi cha pili muunganiko wetu uliimarika, kasi iliongezeka iliyochangiwa na wachezaji vijana na wazoefu,” amesema Robertinho.

Robertinho pia amewasifu Vipers kwa mchezo mzuri na walitupa upinzani mkubwa muda wote lakini sisi tumefanikiwa kupata ushindi.

“Haikuwa mechi rahisi, Vipers walikuwa washindani, wamecheza vizuri lakini tulizijua mbinu zao tukafanikiwa kuwathibiti,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER