Alichosema Pablo baada ya mechi ya jana

Baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema kwa sasa tunaweka nguvu kwenye mechi zetu mbili za nyumbani na moja ya ugenini.

Pablo amesema tumekuwa timu ya kwanza kwenye kundi letu kupata alama ugenini ambayo imeongeza hali ya kupambana ili tufuzu hatua inayofuata.

Akizungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema kipindi cha kwanza tuliwaacha Berkane wacheze lakini tulivyorudi cha pili tuliongeza kasi ya mashambulizi na tulipata nafasi ya kufunga ingawa mpira uligonga mwamba.

“Tumefanikiwa kupata alama moja ugenini na tumekuwa timu ya kwanza kufanya hivyo. Baada ya mechi hii tunarudi nyumbani kujipanga kwa michezo miwili ya nyumbani na mmoja wa ugenini.

“Katika mchezo wa jana tuligawana vipindi wao walikuwa bora cha kwanza nasi tulivyorudi cha pili tulionyesha uwezo mkubwa lakini hatufanikiwa kupata bao,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER