Alichosema Kocha Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua pointi tatu muhimu.

Matola amesema tunategemea kukutana upinzani mkubwa kutoka kwa Kagera licha yakuwa tayari wameshuka daraja lakini tupo tayari kuwakabili ili kufanikisha malengo tuliyojiwekea.

Matola ameongeza kuwa kutokana na ugumu wa ratiba ambao unatufanya kucheza kila baada ya siku mbili tunategemea kufanya mabadiliko ya kikosi ili kuwapumzisha baadhi ya wachezaji.

“Ni kweli Kagera wameshuka daraja lakini tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwao lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunapata alama zote tatu,” amesema Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema wapo tayari kuhakikisha tunapambana hadi mwisho ili kupata alama tatu.

Ally ameongeza kuwa tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Kagera kutokana nakuwa na wachezaji bora licha yakuwa tayari wameshuka daraja.

“Haitakuwa mechi nyepesi, Kagera ni timu imara na ina wachezaji wazoefu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua pointi tatu muhimu,” amesema Ally.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER