Alichosema Kapombe baada ya kuwasili Algeria

Baada ya kuwasili salama nchini Algeria mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo ya walimu kwenye mazoezi ili kufanya vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine siku ya Jumapili.

Kapombe amesema siku mbili za mazoezi ambazo watazipata watazitumia vizuri kuhakikisha tunapata matokeo chanya ugenini.

Akizungumza kuhusu hali ya hewa ya Algeria, Kapombe amesema ni baridi kali lakini siku zilizobaki kabla ya mchezo zitasaidia kuwafanya kuzoea mazingira.

“Hali ya hewa ni baridi kali lakini tuna siku mbili za kufanya mazoezi pamoja na kuzoea mazingira tunaamini hadi kufika siku ya mchezo tutakuwa tumeshazoea,” amesema Kapombe.

Kikosi chetu kimewasili salama hapa Algeria usiku huu na kesho kitaanza programu ya mazoezi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER