Alichosema Benchikha kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amesema tutaingia katika mchezo wa kesho wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kwa lengo la kupambana kwa ajili ya kupata matokeo chanya na kufuzu nusu fainali.

Pamoja na ubora walionao Al Ahly na historia yao kwenye michuano hii bado hatuogopi na tutacheza soka letu la kawaida.

Benchikha ameongeza kuwa tmekuja Misri kushindana na tunajua mechi itakua ngumu lakini amewaambia wachezaji watumie kila nafasi watakayopata kuhakikisha tunapata mabao.

“Hatujaja kufungwa hapa Misri, kama tungejua tunakuja kufungwa tusingekuja kabisa, tumekuja kushindana wala hatuhofii chochote. Itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuwakabili,” amesema Benchikha.

Kwa upande wake mlinzi wa kati Che Fondoh Malone amesema licha ya kucheza ugenini bila mashabiki wetu lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.

“Kuna tofauti ya kucheza nyumbani na ugenini lakini mpira ni ule ule mashabiki wao hawawezi kutuathiri chochote, sisi tutajikita na yale yanayotokea Uwanjani tuu,”: amesema Che Malone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER