Alichokisema Kapombe kabla ya kupaa kuelekea Kagera

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, amesema maandalizi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Kaitaba yanaendelea vizuri na anaamini tutarejea na alama zote tatu.

Kapombe amesema hayo akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), muda mfupi kabla ya kuondoka na wachezaji wenzake kuelekea mkoani Kagera.

Kapombe amesema kuwa anafahamu Kagera imetoka kupata sare katika mchezo uliopita ugenini dhidi ya Azam FC hivyo tutaingia uwanjani kwa tahadhari zote.

Mlinzi huyo amekiri mchezo utakuwa mgumu kwani Kagera ni timu nzuri hasa inapokuwa nyumbani lakini tumejiandaa kupambana kuhakikisha tunashinda.

“Tunajua mechi itakuwa ngumu Kagera ni timu nzuri hasa inapokuwa nyumbani lakini tumejiandaa kupambana kuhakikisha tunashinda. Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho tutafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani Jumamosi,” amesema Kapombe.

Kapombe amewaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi uwanjani siku hiyo ili kutupa sapoti na hatimaye tupate ushindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER