Ajibu, Banda, Gadiel kuanza dhidi ya Geita

Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu na winga Peter Banda wamepangwa kuanza katika kikosi kitakachoikabili Geita Gold leo katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Ajibu na Banda mara nyingi wamekuwa wakitokea benchi na kubadili mchezo kitu ambacho kimemfanya Kocha Pablo Franco kuwaanzisha.

Ajibu amepangwa kama winga wa kushoto wakati Banda akiwa kulia kuwasaidia Nahodha John Bocco na Kibu Denis ambao wataongoza mashambulizi.

Mlinzi wa kushoto Gadiel Michael pia ameanza katika mchezo wa leo akichukua nafasi ya Mohamed Hussein ambaye yupo benchi huku Kennedy Juma akiingia kikosini.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20) Peter Banda (7), Rally Bwalya (8), John Bocco (22), Kibu Denis (38), Ibrahim Ajibu (10)

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Mohamed Hussein (15), Pascal Wawa (6), Mzamiru Yassin (19), Hassan Dilunga (24), Medie Kagere (14), Bernard Morrison (3)Yusuph Mhilu (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER