Ahoua Jean Charles ni Mnyama

Tumefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili.

Ahoua mwenye umri wa miaka 22 tumemsajili kutoka klabu ya Stella Club d’Adjamé ya nchini kwao Ivory Coast.

Katika msimu wa 2023/24 Ahoua ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MVP) na klabu yake huku akifunga mabao 12 na kutoa ‘assist’ tisa.

Ahoua anasifika kwa kufunga mabao kutoka umbali mrefu, kuchezesha timu pamoja kutengeneza nafasi kwa wenzie.

Tunategemea mambo makubwa kutoka kwa Ahoua kwa kushirikiana na nyota wengine tuliowasajili pamoja na wale waliokuwepo kikosini.

Kuelekea msimu wa Ligi 2024/25 tumekuja na utaratibu mpya kwenye usajili wa kuingiza wachezaji bora wenye uwezo na umri mdogo ili kujenga timu imara ya muda mrefu.

Ahoua anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa baada ya Lameck Lawi, Joshua Mutale na Steven Mukwala.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER