Kiungo mshambuliaji, Jean Charles Ahoua amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa 5-1 tuliopata dhidi ya Pamba Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa KMC.
Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 16 kwa mkwaju wa penati baada ya Joshua Mutale kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Ahoua alitupatia bao la pili kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja anafunga baada ya Mutale kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18.
Ahoua alitupatia bao la tatu dakika ya 47 kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi iliyopigwa na Elie Mpanzu na kukamilisha hat trick.
Leonel Ateba alitupatia bao la nne dakika ya 80 baada ya kumalizia mpira uliokolewa na mlinda mlango wa Pamba, Kamara kabla ya kumkuta mfungaji.
Ateba alitupatia bao la tano dakika ya 84 kwa shuti kali nje ya 18 lililotinga wavuni moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango Kamara.
Methew Momanyi aliwapatia Pamba bao la kufutia machozi dakika ya 86 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa kati.
Kiungo mshambuliaji Hamad Majimengi alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya tatu ya nyongeza kufuatia kutoa lugha isiyofaa kwa mwamuzi wa mchezo Shomari Lawi.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 25 tuliendelea kubaki nafasi ya pili.
X1: Camara, Kapombe (Kibu 55′), Zimbwe Jr, Hamza (Che Malone 45′) Okajepha, Mpanzu, Ngoma (Fernandez 55′), Ateba, Ahoua (Nouma 55′) Mutale (Chasambi 70′)
Waliionyeshwa kadi: Hamza 45′
X1: Kamara, Kunambi, Abraham (Ibrahim 82′), Sebo, Omary, Mwashinga, Zabona (Kaseke 66′) Kasindi (Majimengi 67′), Tegisi, Shassiri (Madeleke 67′) Yonta
Waliionyeshwa kadi: Kamara 45+5′, Abdula 49′ Nahimana 65′ Majimengi nyekundu 90+3′