Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema tumeweka kiingilio kidogo kwenye mchezo dhidi ya CS Sfaxien kwakuwa tunahitaji mashabiki wajitojeze kwa wingi uwanjani.
Mchezo dhidi ya CS Sfaxien ambao utakuwa ni watatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika utapigwa Jumapili ya Disemba 15, saa 10 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ahmed amesema kiingilio cha chini kitakuwa Shilingi 3000 ambacho kila Mwanasimba ana uwezo wa kumudu kulipa na malengo yetu ni kuhakikisha Uwanja unajaa.
Ahmed amesema tukijitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa hakuna namna yoyote CS Sfaxien watachomoka.
“Tupo hapa kwa ajili ya dhumuni moja ya kuhakikisha tunaujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili. Wanasimba kwa umoja wetu tukijitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji tuna uhakika wa kupata pointi tatu nyumbani,” amesema Ahmed.
Hivi hapa Viingilio kamili vilivyotangazwa:
Mzunguko Sh. 3000
Machungwa Sh. 5000
VIP C Sh. 10,000
VIP B Sh. 20,000
VIP A Sh. 30,000