Abdulrazack Hamza aitwa Taifa Stars

Baada ya kuonyesha kiwango safi tangu kuanza kwa msimu mlinzi wa kati Abdulrazack Hamza ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Stars inajiandaa na mechi mbili za kufuzu fainali za Afrika (AFCON) dhidi DR Congo ambazo ya kwanza itapigwa Oktoba 10 ugenini na marudiano itakuwa Oktoba 15.

Hamza amekuwa chaguo la kwanza la kocha Fadlu Davids kitu kilicholifanya benchi la ufundi la Stars kumuona na kumpa nafasi.

Nyota wengine kutoka kwenye kikosi chetu walioitwa kwenye kikosi cha Stars ni mlinda mlango Ally Salim, nahodha Mohamed Hussein na Kibu Denis.

Mlinda Moussa Camara nae amejunuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Guinea.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER