Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaoanza saa 10 jioni.
Wachezaji wote waliosafiri wamefanya mazoezi na jambo jema ni kwamba hakuna aliyeumia hivyo watakuwa tayari kwa mchezo wa kesho.
Morali ya wachezaji ipo juu na tutaingia katika mchezo tukiwa na lengo moja la kutafuta alama tatu muhimu ugenini.
Tunajua mchezo utakuwa mgumu na tunawaheshimu Geita kutokana na ubora walio nao lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.