Kocha Mkuu Pablo Franco amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting ukilinganisha na kile kilichoanza na Namungo FC, Mei 3.
Pablo amewaanzisha walinzi Gadiel Michael na Pascal Wawa pamoja na kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho ambao hawakuanza mchezo uliopita.
Medie Kagere ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji akipata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Peter Banda, Kibu Denis na Sakho.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Henock Inonga (29), Pascal Wawa (6), Jonas Mkude (20), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Pape Sakho (10).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Yusuf Mhilu (27), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Jimmyson Mwanuke (21).