Tupo tayari kwa ‘battle’ la Wagosi Mkwakwani leo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuikabili Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaoanza saa 10 jioni.

Kikosi kimewasili jijini Tanga juzi Jumanne na wachezaji wote waliosafiri wako kwenye hali nzuri tayari kuipambania timu kupata alama tatu.

Baada ya mazoezi ya mwisho tuliyofanya jana jioni katika Uwanja wa Mkwakwani hakuna mchezaji yeyote aliyepata maumivu hivyo benchi la ufundi litakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

Tunafahamu tupo katika mzunguko wa pili wa ligi na kila timu inataka kushinda ili kumaliza vizuri msimu nasi tumejipanga kuhakikisha tunashinda kila mchezo ili kutetea ubingwa wetu.

ALICHOSEMA PABLO KUELEKEA MCHEZO WA LEO

Kocha Mkuu Pablo Franco amekiri kuwa hakutapata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo kutokana na ratiba kuwa ngumu lakini tutahakikisha tunapambana mpaka mwisho ili tupate alama tatu.

Pablo ameongeza kuwa anaamini mchezo utakuwa mzuri na utaamuliwa na ubora wa timu uwanjani na si matumizi makubwa ya nguvu.

“Ratiba inatubana, juzi tumetoka kucheza mechi ngumu ya kimataifa jana tumefanya mazoezi mepesi asubuhi mchana tukaanza safari ya kuja huku. Kiuhalisia ni ratiba ngumu lakini tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunapata ushindi,” amesesema Pablo.

GADIEL ATOA NENO

Mlinzi wa kushoto Gadiel Michael amesema tutaingia uwanjani kwa kuiheshimu Coastal na tunajua itakuwa mechi ngumu ukizingatia tupo ugenini lakini tupo tayari kuipigania timu kupata pointi tatu muhimu.

“Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu, Coastal ni timu nzuri na ipo nyumbani kwa hiyo tutahakikisha tunapambana kupata alama tatu, kwa sasa kila mchezo ni fainali kwetu,” amesema Gadiel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER