Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa uwanjani hapo.
Kikosi kimewasili jijini Tanga jana usiku na wachezaji walipumzika hadi leo jioni ambapo wamefanya mazoezi ya mwisho.
Morali ya wachezaji ipo juu na nyota wote waliokuja jijini hapa wako kwenye hali nzuri hakuna aliyepata majeraha yoyote baada ya mazoezi ya leo.
Tutaingia katika mchezo wa kesho tukijua hautakuwa rahisi, Coastal ni timu nzuri na inacheza katika uwanja wao wa nyumbani lakini lengo ni kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu.