Baada ya kukamilika kwa droo ya hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kupangwa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini Kocha Mkuu Pablo Franco amekiri itakuwa mechi ngumu.
Pablo amesema Pirates wanacheza soka safi na wana wachezaji wazuri kwa hiyo tutapaswa kuwa makini katika mchezo wa nyumbani kwa kuzitumia vizuri nafasi tutakazopata.
Pablo ameongeza kuwa kwenye michuano hii kila hatua ugumu unaongezeka lakini tunapaswa kupambana vilivyo ili tuvuke hatua inayofuata.
“Tumepangwa na timu ngumu, tunapaswa kuwa makini na kutumia vizuri nafasi tutakazopata katika uwanja wa nyumbani. Hatupaswi kufanya makosa mengi ili tuwe salama.
“Tunapaswa kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huo mgumu na tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunavuka hatua hii,” amesema Pablo.