Droo ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali imekamilika na tumepangwa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Katika droo hiyo iliyofanyika nchini Misri tumepangwa kuanzia nyumbani ambapo mchezo wa kwanza utafanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 17 na marudio itakuwa Aprili 24 nchini Afrika Kusini.
Pirates walikuwa vinara wa kundi B ikiwa na alama 13 mabao 10 wakati Simba tumemaliza nafasi ya pili katika kundi letu la B tukiwa na alama 10.