Usalama siku ya mchezo ni asilimia 100

Uongozi wa klabu umewatoa hofu mashabiki ambao wamepanga kujitokeza katika mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie ambapo utapigwa saa nne usiku kwa sababu ulinzi umeimarishwa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha kila shabiki atakayekuja uwanjani anarejea salama nyumbani kwake.

Ahmed amesema mara kadhaa kumekuwa na vitendo vya uhalifu hasa nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini ulinzi umeimarishwa na mashabiki wote watakaokuja watarejea majumbani kwao salama.

“Kwanza niwatoe hofu mashabiki wetu ambao wamepanga kujitokeza uwanjani waje bila wasiwasi sababu ulinzi utakuwa umeimarishwa na kila mtu atakuwa salama. Wanasimba msiwe na hofu njooni Benjamin Mkapa,” amesema Ahmed.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Tanzania (TADU), Jaeka Mdami amesema daladala za kwenda sehemu yoyote jijini Dar es Salaam zitapatikana na nauli itakuwa ile ile ya kawaida.

“Kuhusu usafiri utapatikana nje ya uwanja wa Benjamin na daladala za kwenda sehemu yoyote Dar es Salaam zitapatikana kwa hiyo mashabiki msiwe na hofu ya usafiri,” amesema Mdami.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER