Katika kuonyesha tumedhamiria kushinda na kutinga Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika leo tumezindua kampeni ya hamasa kwa mashabiki ili kujitokeza kwa wingi uwanjani Jumapili katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie.
Kampeni hiyo imezinduliwa na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu katika kituo cha mabasi cha John Magufuli huku wenyeji wetu wakiwa Tawi la Wekundu wa Terminal.
Mwenyekiti Mangungu amewashukuru viongozi wa matawi yaliyojiunga pamoja kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa ili kuhamasisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumapili.
Mangungu amesema kuwa yeye binafsi atatoa tiketi 200 kwa vikundi mbalimbali au matawi ya klabu kwa ajili ya kuongeza hamasa ambapo utaratibu mzuri utawekwa jinsi ya kugawiwa.
“Lengo ni moja kuhakikisha tunashinda na kutinga robo fainali ya michuano hii, binafsi nitatoa tiketi 200 kupitia vikundi na matawi ili kuongeza hamasa,” amesema Mangungu.
Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema Ijumaa kutakuwa na kampeni nyingine kubwa ambapo tutapanda treni kuanzia Kamata hadi Pugu ambapo humo ndani kutakuwa na burudani mbalimbali.
“Hii haiishii leo, kesho kutwa Ijumaa tutakosi behewa kutoka Kamata Kariakoo kuelekea Pugu lengo ni kuhakikisha tunahamasisha mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani,” amesema Ahmed.
2 Responses