Nahodha wa timu John Bocco, ameomba radhi kwa mashabiki na viongozi kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa ASEC Mimosas katika mchezo wa tano wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa nchini Benin.
Bocco amesema hali kama hii hutokea kwenye soka wakati mwingine timu bora uwanjani hupoteza mechi kitu ambacho tutahakikisha hakijirudii.
Amesema matokeo yamewaumiza pia wachezaji lakini wameyasahau na kujipanga kwa mchezo wa mwisho dhidi ya US Gendarmerie.
Bocco ameahidi kuwapa furaha Wanasimba katika mchezo huo ambao utapigwa Aprili 3 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
“Nichukue fursa hii kuwaomba radhi mashabiki, viongozi na Wanasimba wote kwa matokeo mabaya tuliyopata. Hata sisi wachezaji tumeumia lakini ndiyo mpira.
“Tunajipanga kwa mechi yetu ya mwisho ya nyumbani ninaamini tutawapa furaha mashabiki wetu kwa kutimiza lengo la kuingia robo fainali,” amesema Bocco.
One Response
Peter Banda is so talented .may he keep up the spirit