Kocha Mkuu Pablo Franco, amekiri kuwa hatukucheza vizuri katika mchezo wa jana wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas na kusababisha kupoteza mechi.
Pablo amesema kulikuwa na makosa ya wachezaji mmoja mmoja na timu pia hivyo ilikuwa lazima tuadhibiwe hasa tunapocheza ugenini.
Pablo amesema kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwetu wenyeji walitawala na kupata mabao mawili lakini cha pili tulirudi vizuri na kufanya mashambulizi ingawa tulipoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Raia huyo wa Hispania ameongeza kuwa kama kocha anakubali kubeba lawama zote lakini amewataka wachezaji waonyeshe kama wanacheza timu kubwa na wapambane uwanjani zaidi ya walivyofanya jana.
“Hatukucheza vizuri, ni tofauti na matarajio yetu. Kipindi cha kwanza ASEC walitawala na kupata mabao mawili cha pili tulirudi na tulipoteza nafasi za kufunga.
“Kama kocha nakubali kubeba lawama kwa kilichotokea lakini wachezaji wangu nao wanapaswa kuhakikisha wanapambana sababu wanacheza timu kubwa,” amesema Pablo.
One Response