Kikosi chetu kimewasili salama nchini Benin mchana huu tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Jumapili saa moja usiku katika Uwanja wa Generali Mathieu Kérékou.
Baada ya kikosi kufika wachezaji watapumzika kwa saa chache kabla ya kwenda mazoezini jioni kuweka miili sawa (recovery).
Tutaingia katika mchezo Jumapili tukiwa na lengo la kutafuta alama tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kuingia robo fainali ya michuano hii.