Chama, Bwalya, Banda waitwa timu zao za taifa

Nyota wetu watatu wa Kimataifa wameitwa katika timu zao za taifa wakati ligi zikisimama kupisha mechi za kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Clatous Chama na Rally wameitwa Timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ ambayo itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Machi 25) na Guinea (Machi 29).

Winga Peter Banda amejumuishwa katika kikosi cha Malawi chini ya umri wa miaka 23 kitakachosafiri kwenda nchini Uturuki kushiriki michuano maalumu.

Michuano hiyo inayoitwa Antalya Cup itafanyika katika mji wa Antalya itaanza Machi 24 na kumalizika Machi 28 na Banda atakuwa huko muda wote.

Baada ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Machi 20 nchini Benin wachezaji hao wataruhisiwa kujiunga na timu zao za taifa.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER