Alichosema Zimbwe Jr kuelekea mchezo wa kesho

Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ameweka wazi kuwa wachezaji wapo kamili kuikabili RS Berkane katika mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Zimbwe Jr amesema makosa tuliyofanya katika mchezo uliopita nchini Morocco benchi la ufundi limeyafanyia kazi na kesho ni zamu yetu kupata ushindi.

Mlinzi huyo wa kushoto ameongeza kuwa moja ya sababu iliyotufanya kupoteza mchezo uliopita kule Morocco ni uwepo wa mashabiki ambao walikuwa wanaisapoti kwa wingi timu yao hivyo kesho itakuwa zamu yetu kupata nguvu ya mashabiki.

“Kwa upande wa wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunajua umuhimu wa kushinda mechi hii pia tunataka kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza benchi la ufundi iliyaona na tumeyafanyia kazi mazoezini. Kikubwa nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kutupa sapoti tunaamini tutawapa furaha,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER