Pablo: Tunahitaji kuichapa Berkane nyumbani

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesisitiza kuwa tunahitaji kupata alama tatu katika mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Pablo amesema tunaenda kukutana na timu ngumu ambayo ilitufunga kwao hivyo nasi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika uwanja wa nyumbani.

Pablo ameongeza kuwa tumekuwa na wiki nzuri ya mazoezi na wachezaji wengi waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini na wameongeza nguvu kuelekea mchezo wa kesho.

“Tupo katika uwanja wa nyumbani tunahitaji kupata alama tatu. Tunaenda kukutana na timu bora ambayo ilitufunga kwao lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kwetu.

“Tumepata muda mzuri wa kujiandaa, tulikuwa na wiki ya kufanya mazoezi wachezaji wapo kwenye hali nzuri tunaamini tutafanya vizuri kesho,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER