Kikosi chetu kitaingia kambini baada ya mazoezi ya leo jioni kujiandaa na mchezo wa nne wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.
Mchezo huo ni muhimu kwetu na tunahitaji kupata alama tatu nyumbani ambazo zitatuweka katika nafasi nzuri kwenye kundi letu.
Maandalizi ya mchezo yanaendelea na tayari viingilio vya mchezo vimeshatangazwa mapema ili mashabiki wanunue tiketi kupitia kwenye mitandao na kwenye vituo.
Viingilio vipo kama ifuatavyo
Mzunguko Sh 3,000
VIP B na C Sh. 20,000
VIP A Sh 30,000
Platinum Sh 150,000
Uongozi unawasihi mashabiki kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mchezo.