‘Tumezitafuna zabibu za Dodoma’

Tumefanikiwa kukusanya alama tatu muhimu baada ya kuifunga Dodoma Jiji mabao 2-0 Katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tulianza mechi kwa kasi ya kawaida huku tukitengeneza nafasi lakini ufanisi wetu mbele ya lango ulikuwa mdogo huku Dodoma wakicheza zaidi nyuma.

Nahodha John Bocco alishindwa kuendelea na mchezo dakika ya 24 baada ya kugongwa na mchezaji wa Dodoma nafasi yake ikachukuliwa na Medie Kagere.

Dakika ya 56 Clatous Chama alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi mmoja wa Dodoma kuunawa mpira ndani ya 18.

Medie Kagere alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 75 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Peter Banda.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Pape Sakho, Chama, Banda na Erasto Nyoni na kuwaingiza Rally Bwalya, Jimmyson Mwanuke, Taddeo Lwanga na Kibu Denis.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER