Droo ya hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) imekamilika na tumepangwa na Pamba FC inayoshiriki Championship kutoka jijini Mwanza.
Mchezo huo utapigwa kati ya Aprili 8 hadi 13 ambapo sisi ndio tutakuwa wenyeji hivyo mtanange utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mshindi kati yetu na Pamba atakutana na mshindi wa Yanga na Geita Gold katika mchezo wa Nusu Fainali.
Sisi ndio mabingwa watetezi wa michuano hii na moja ya lengo letu msimu huu ni kuhakikisha tunatetea taji letu.
2 Responses
Lazima tumpige pamba Kisha mtani na hatimae fainali na kuchukua
Naipenda Tanzania naipenda simba