Mshambuliaji nyota wa Timu ya Simba Queens, Opa Clement amechaguliwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) wa mwezi Januari.
Opa amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi chetu akihusika na ushindi kwa asilimia kubwa kwenye kila mchezo.
Katika mwezi Januari, Opa amefunga mabao 10 katika michezo sita tuliyocheza huku akifanikiwa kufunga mabao matatu (hat trick) moja.
Opa atakabidhiwa fedha taslimu Sh 500,000 kutoka kwa wadhamini Rani Sanitary Pad.