Kocha Msaidizi Seleman Matola, amewasifu wachezaji kwa kufuata maelekezo kutoka benchi la ufundi na kusababisha kupatikana kwa ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City.
Matola amesema walijituma kuanzia mwanzo hadi mwisho kuhakikisha tunapata ushindi mnono na hicho ndicho kitu cha kushukuru.
Akizungumzia mchezo huo, Matola amesema tulipanga kuanza kwa kasi kwa kuwakabia juu na kufanikiwa kupata mabao matatu ndani ya dakika 20 za kwanza.
“Kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji kwa jinsi walivyojituma muda wote, tulihitaji ushindi huu na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa.
“Tulipanga kukabia juu na kuanzisha mashambulizi na tulifanikiwa. Kama umeona ndani ya dakika 20 za mwanzo tukawa tumepata mabao matatu na bado naendelea kuwapongeza wachezaji,” amesema Matola.
2 Responses
Hiyo sehemu ya kupiga kura ni wapi sasa?