Tumetinga 16 Bora ASFC kibabe

Ushindi mnono wa mabao 6-0 tuliopata dhidi ya Dar City umetuwezesha kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kishindo

Medie Kagere alitupatia bao la kwanza mapema dakika ya tano baada ya kupokea pasi mpenyezo kutoka kwa Clatous Chama.

Kagere tena alitupatia bao la pili dakika ya 12 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga ambaye alimlamba chenga mlinzi mmoja wa Dar City.

Clatous Chama alitupatia bao la tatu kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni dakika ya 18 baada ya Gadiel Michael kufanyiwa madhambi.

Rally Bwalya alitupia bao la nne dakika ya 21 akimalizia pasi ya Chama akiwa ndani ya 18.

Dakika ya pili ya kipindi cha pili Pascal Wawa alitupatia bao la tano kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kutengewa mpira wa kifua na Erasto Nyoni.

Chris Mugalu alikamilisha karamu ya mabao baada ya kutupia bao la sita dakika ya 79 kufuatia kupokea pasi safi kutoka kwa Dilunga.

Kocha msaidizi Seleman Matola aliwatoa Henock Inonga, Bwalya, Kagere, Yusuf Mhilu na Chama na kuwaingiza John Bocco, Jimmyson Mwinuke, Pascal Wawa, Chris Mugalu na Bernard Morrison.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER