Timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imeendelea kufanya vizuri katika Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuichapa JKT mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Karume.
Mchezo huo ulikuwa mkali huku timu zikishambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi ingawa hazikutumiwa ipasavyo hadi timu hizo zinaenda mapumziko.
Mshambuliaji nyota Michael Joseph, alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 58 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Joseph Mbaga.
Mbaga alitupatia bao la pili dakika ya 71 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa JKT.
Zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo kukamilika Mbaga alitupia bao la tatu baada ya kuwazidi nguvu walinzi wa JKT akiwa ndani ya 18.
Kikosi chetu kimeshinda michezo yote minne tulivyocheza hadi sasa ambayo ni dhidi ya JKU, Ashanti, Cambiaso na wa leo wa JKT.
One Response