Pablo: Tumekuwa na wiki ngumu

Kocha Mkuu Pablo Franco, amekiri tumekuwa na siku tisa ngumu ambazo tumecheza mechi tatu za ugenini zilizotufanya kusafiri umbali mrefu bila matokeo.

Pablo amesema ratiba ilikuwa ngumu ambayo imesababisha wachezaji kuchoka huku wengine wakipata majeraha ambayo yamewafanya kukosa baadhi ya mechi.

Akizungumzia mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar, Pablo amesema timu imebadilika kiuchezaji tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hata hivyo hatukuzitumia.

Amesema kikosi kinarejea jijini Dar es Salaam ambapo tutakuwa na muda mzuri wa kufanya mazoezi na kucheza katika uwanja mzuri hivyo tunaweza kurudi katika ramani ya ushindi.

“Tumekuwa na siku tisa ngumu, tumepata alama moja kati ya tisa, tumecheza mechi tatu ugenini na tumesafiri umbali mrefu hivyo wachezaji hawajapata muda mzuri wa kupumzika na kufanya mazoezi.

“Wakati mwingine katika soka unaweza kucheza tofauti na ulivyotarajia. Kwa sasa tunarudi Dar na malengo yetu ni kuhakikisha tunarudi katika mwenendo wa ushindi ili kurejesha hali ya kujiamini kwa timu na wachezaji,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER