Nyota watakaotuwakilisha dhidi ya Mtibwa leo

Muda mfupi ujao kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi ya NBC utakaoanza saa 10 jioni.

Kocha Pablo Franco amefanya mabadiliko kidogo ya kikosi ambapo mlinzi wa kushoto Gadiel Michael ataanza mbele ya Mohamed Hussein huku Hassan Dilunga akichukua nafasi ya Kibu Denis ambaye ni majeruhi.

Mzamiru Yassin ataanza pamoja na Sadio Kanoute akichukua nafasi ya Jonas Mkude ambaye amebaki jijini Dar es Salaam kutokana na kuwa majeruhi.

Pablo pia ameanza na washambuliaji wawili Chris Mugalu na Medie Kagere ili kuhakikisha tunatumia kila nafasi tutakayopata.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Hassan Dilunga (24), Mzamiru Yassin (19), Chris Mugalu (7), Medie Kagere (14), Pape Sakho (10)

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Bernard Morrison (3), John Bocco (22), Clatous Chama (17), Yusuph Mhilu (27)

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER