Sakho aridhia kumwachia Chama namba 17

Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amekubali kumwachia jezi namba 17 Clatous Chama ambayo alikuwa anaitumia tangu ajiunge nasi katika majira ya kiangazi yaliyopita.

Kabla ya kuondoka na kujiunga na RS Berkane, Chama alikuwa anavaa jezi namba 17 ambayo ndiyo inamtambulisha.

Sakho sasa atavaa jezi namba 10 ambayo imeachwa na Ibrahim Ajibu aliyejiunga na Azam FC.

Baada ya kumkabidhi Chama jezi hiyo, Sakho amesema amefanya hivyo kwa heshima ya fundi huyo kutokana na makubwa aliyofanya ndani ya timu.

“Nimekubali kumwachia namba 17 Chama kutokana na heshima niliyo nayo kwake, amefanya makubwa ndani ya timu. Nitatumia jezi namba 10 kuanzia sasa,” amesema Sakho.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Naitakia kila la kheri Club yangu ya Simba Sport Club kwa mchezo wa leo 17/01/2022 na Mbeya City ya Jijini Mbeya. Nina imani na kikosi kitakachoanza na tutaibuka na ushindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER