Tumelibeba…

Baada ya kupita muda mrefu bila kutwaa taji la Michuano ya Mapinduzi hatimaye tumefanikiwa baada ya kuifunga Azam FC bao moja mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar.

Katika michuano hii tumeweka rekodi ya kumaliza bila kuruhusu bao hata moja huku ukiwa ni ubingwa wa nne kwetu.

Mchezo ulianza kwa kasi kubwa timu zikishambuliana kwa zamu lakini ulichezwa zaidi katikati ya uwanja huku washambuliaji Medie Kagere na Rogers Kola wakiachwa peke yao.

Walinda mlango Aishi Manula na Mathias Kigonya hawakuwa bize sana kipindi cha kwanza lakini mashambulizi machache waliyokutana nayo yalikuwa hatari.

Kagere alitupatia bao la kwanza dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati baada ya Pape Sakho kufanyiwa madhambi na Kigonya ndani ya 18.

Baada ya bao hilo Azam waliongeza kasi kutaka kusawazisha lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara kuondoa hatari zote.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Rally Bwalya, Kagere, Sakho na Kibu Denis na kuwaingiza Bernard Morrison, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Pascal Wawa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER