Tuko tayari kwa fainali

Leo saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Aman, Visiwani Zanzibar kikosi chetu kitashuka kuikabili Azam FC katika mchezo wa Fainali ya Michuano ya Mapinduzi.

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, hakuna ambaye atakosekana kwa sababu yoyote iwe ni adhabu ya kadi au majeraha.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho jana usiku katika Uwanja wa Amaan na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo huo wa fainali.

PABLO atoa neno

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema muda umefika wa kubadili historia katika mashindano haya. Tumekuwa hatuna bahati na michuano hii lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Pablo amesema anaamini mchezo utakuwa mzuri kama ule wa nusu fainali dhidi ya Namungo kutokana na timu zote kucheza mpira wa chini usio na matumizi makubwa ya nguvu.

“Tangu mara ya kwanza nilivyokuja hapa Zanzibar nilisema malengo yetu ni kutwaa ubingwa, leo ni fainali tupo tayari kupambana kuhakikisha tunatwaa taji. Tunajua hatuna bahati na michuano hii lakini leo tunataka kuvunja mwiko,” amesema Pablo.

KAPOMBE: WACHEZAJI WOTE TUKO TAYARI

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Shomari Kapombe, amesema kila mchezaji yuko tayari kwa ajili ya fainali na lengo ni moja tu, kutwaa taji.

“Tunajua kila tukifika fainali huwa tunapoteza. Katika miaka ya karibuni tumekuwa hatuna bahati na fainali ya michuano hii lakini leo tutabadili kila kitu kwa kuchukua ubingwa,” amesema Kapombe.

MIAKA SABA TAJI MOJA

Katika miaka saba iliyopita tumefanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo mara tano lakini tumeshinda ubingwa mara moja pekee kitu ambacho tunataka kuvunja mwiko leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER